1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza la usalama la umoja wa mataifa lashutumu mauaji nchini Iraq.

9 Julai 2005

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeshutumu mauaji dhidi ya mjumbe wa ngazi ya juu katika ubalozi wa Misr nchini Iraq , Ihab el Sharif.

Katika taarifa ya pamoja , baraza hilo limeshutumu mashambulizi yote dhidi ya wafanyakazi wa kiraia wa kimataifa nchini Iraq.

Tawi la mtandao wa kigaidi wa al Qaeda nchini Iraq limesema kuwa limemuua el Sharif baada ya kumteka nyara mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wakati huo huo , Misr imesema kuwa itapunguza wafanyakazi wake katika ubalozi huo mjini Baghdad kufuatia kuuwawa kwa el-Sharif.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Misr Ahmed Aboul Gheit amesema upunguzaji huo ni kwa ajili wa kuwalinda wafanyakazi wa ubalozi huo.

Lakini wizara ya mambo ya kigeni ya Iraq imeyataka mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kutoyumbishwa na ghasia hizo za wapiganaji wa chini kwa chini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW