1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa latakiwa litume majeshi Darfur

15 Septemba 2006
Kombe la mabingwa wa bara ulaya.
Kombe la mabingwa wa bara ulaya.Picha: dpa

Mchezaji filamu, George Clooney jana aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ikiwa halitapeleka vikosi vya kulinda usalama katika eneo la Darfur nchini Sudan, mamilioni ya watu watakufa katika kile alichokiita, mauaji ya kwanza ya halaiki ya karne ya 21.

George Clooney ameonya juu ya hali mbaya ya kibinadamu huko Darfur.

´Hali si nzuri bali inaendelea kuwa mbaya zaidi na ni jumuiya ya kimatiafa inayoweza kutusaidia. Ifikapo Oktoba mosi, sio waasi wa Janjaweed watakaokuwa wakiua na kuwabaka watu. Waasi wa kundi la SLA nao pia wanaua watu. Bila kulindwa, wafanyakazi wote wa kutoa misaada ya kiutu wataondoka mara moja na wakimbizi milioni 2.5 wanaotegemea misaada hiyo, watakufa.´

Clooney alikuwa akiuhutubia mkutano wa baraza la usalama la usalama la Umoja wa Mataifa ambao uliandalindaliwa na wakfu wa Elie Wiesel. Mkutano wa baraza hilo hakuwa rasmi.

Wiesel, aliyenusirika wakati wa mauaji ya halaiki ya wayahudi na ambaye ni mshindi wa tunzo la amani la Nobel, aliwatolea mwito wanachama wa baraza la usalama wachukue hatua za dharura kuzuia mauaji huko Darfur.

´Kadri tunavyolijadili swala hili, watu wanakufa. Msisubiri Sudan iwaalike au ikubali mutume majeshi. Ikikubali ni vyema, ikikataa, nendeni bila kuogopa. Waasi hawasubiri. Wazuieni.´

Marekani imewalaumu washirika wake kwa kutofanya lolote kuilazimisha Sudan ikubali wanajeshi wa kulinda amani wapelekwe Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW