1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Islam Karimov anapinga uchunguzi wa Umoja wa Mataifa

20 Mei 2005

Afisa mmoja wa Umoja wa mataifa amefahamisha kwamba rais wa Uzbekistan bwana Islam Karimov amemwambia katibu mkuu Kofi Annan kwamba hapendelei Umoja wa Mataifa ufanye uchunguzi juu ya matukio ya wiki jana nchini Uzbekistan ambapo mamia ya watu waliauawa katika mapambano baina ya wanajeshi na wapinzani.

Umoja wa Mataifa unataka uchunguzi huo ufanyike kutokana na madai kwamba majeshi ya usalama yalifanya mauaji.

Baadhi ya jumuiya za haki za binadamu zinasema kwamba raia wapatao alfu moja waliuawa katika miji ya Andijan na Paakh-taabad katika mapambano na majeshi ya usalama.

Serikali ya Uzbekistan imekanusha madai kwamba majeshi yake ya usalama yaliwashambulia waandamanaji, lakini imesema kwamba majeshsi hayo yaliwaua waasi zaidi ya 130 wa kiislamu.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW