1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Israel haikulaaniwa na Umoja wa Mataifa

28 Julai 2006

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York limetoa hati inayosema kuwa Umoja wa Mataifa umeshtushwa na kuhuzunishwa na shambulio la Israel kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.Shambulio hilo siku ya Jumanne liliwaua walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon.Hati hiyo lakini kwa sababu ya mbinyo wa Marekani,haikuilaani Israel.Wanachama wa Baraza la Usalama wamesema Israel inapaswa kufuata kikamilifu sheria za kimataifa kuhusu tume za waangalizi na ihakikishe kuwa wafanya kazi wa Umoja wa Mataifa hawakabiliwi na mashambulio.Hati hiyo pia imeitaka Israel ifanye uchunguzi kamilifu na itangaze matokeo yake.China imekosoa vikali utii wa Marekani kuhusu Israel. Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa,Wang Guangya amesema Marekani kwa utiifu wake imechafua mazingira katika umoja huo na kwa hivyo kila lawama iliyotolewa dhidi ya Israel ilipunguzwa makali.China ilipoteza mwanajeshi wake mmoja baada ya kituo cha Umoja wa Mataifa kushambuliwa na Israel kusini mwa Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW