1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Jan Egeland atazamiwa kukutana na Joseph Kony wa LRA

12 Novemba 2006

Mkuu wa wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia miradi ya kiutu,Jan Egeland anatazamiwa kukutana na viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Uganda,LRA.Vile vile huenda akakutana na Joseph Kony anaetafutwa sana na jumuiya ya kimataifa.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,mkutano huo huenda ukafanywa leo hii sehemu za ndani,kusini mwa Sudan,karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,ambako Kony na makamanda wengine wa LRA wanajificha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW