New York. Jeshi la umoja wa mataifa nchini DRC laongezewa muda.
14 Aprili 2007Matangazo
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha kwa kauli moja kurefusha muda wa ujumbe wa jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani kwa mwezi mmoja katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , ujumbe ambao una wanajeshi karibu 18,000.
Baraza hilo liliidhinisha pia kurefusha ujumbe huo kwa miezi miwili mwezi wa Februari.
Hii ilikuwa na nia ya kumpa katibu mkuu Ban Ki-moon muda wa kuweza kutoa uwezekano wa mabadiliko katika muda wa jeshi hilo la kulinda amani kufuatia uchaguzi uliofanyika mwaka jana.
Wajumbe wa baraza hilo wamekuwa wakifanyia kazi azimio jipya ambalo litaruhusu ujumbe huo kukaa muda mrefu zaidi, lakini wanadiplomasia wa Marekani wamesema kuwa baraza la Congress linahitaji muda zaidi ili kutoa baraka zake.