1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Kofi Annan, alaani mauaji ya wakili katika kesi ya Saddam

9 Novemba 2005

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan, amelaani mauaji ya mawakili wawili katika kesi ya kiongozi wa zamani wa Irak, Saddam Hussein.

Abdel Mohamed Abbas, wakili wa aliyekuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa Saddam, Taha Yassin Ramadan, aliuwawa hapo jana mjini Baghdad wakati watu waliokuwa na bunduki walipolifyatulia risasi gari lake. Wakili mwenzake, Thamer Hamoud al-Khuzaie, anayemtetea kakaye Saddam, Barzan Ibrahim al-Tikriti, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

Tukio hilo linafuatia mauaji ya wakili Saadun Janabi, aliyeuwawa na watu wasiojulikana baada ya kutekwa nyara mnamo Oktoba 20, siku moja baada ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya Saddam.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW