1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-York: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ...

26 Desemba 2003

ameutaja mwaka huu unaomalizika wa 2003,kua mwaka ulioshuhudia mashaka makubwa kabisa katika historia ya miaka 58 ya umoja wa mataifa.Katika hotuba yake ya mwaka mpya,katibu mkuu Kofi Annan amewasihi walimwengu wajishughulishe zaidi hivi sasa na matatizo mengine muhimu yanayoweza pia kuhatarisha amani.Amedhukuru malengo ya Millenium,yanayotarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2015.Malengo hayo ni pamoja na kupambana na umasikini,njaa na maradhi.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofiu Annan amesema ahadi zilizotolewa wakati wa mkutano wa Millenium zinabidi zitekelezwe kivitendo hivi sasa.Amesisitiza sehemu ndogo tuu ya fedha zinazotumiwa kutengeneza silaha zingetosha kuyafikia malengo hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW