1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Kenya yaiombea msaada Somalia

27 Septemba 2006

Kenya imetowa ombi zito kwa serikali za dunia hapo jana kwa haraka kuisaidia Somalia yenye machafuko venginevyo dunia nzima itazidi kuwa mahala pa hatari.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Raphael Tuju ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba Somalia karibu inakufa na wanaliona hilo na kwamba wamekuwa wakilijuwa hilo kwa miaka 16 na huu ni wakati wa kutuma msaada wa kuiokowa nchi hiyo.

Amesema msaada wa kibinaadamu hivi sasa utazaa matokeo mazuri na ya haraka kuliko kuingilia kati kijeshi nchi hiyo na kwa gharama nafuu zaidi kuliko kutuma vikosi kuwaandama watu wahalifu katika nchi hiyo isiokuwa na utawala wa sheria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW