1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kifo cha Hariri kichunguzwe upya

25 Machi 2005

Umoja wa Mataifa umetoa muito wa kufanywa uchunguzi huru kuhusu mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafiq al-Hariri.Ripoti iliyotolewa na tume maalum ya Umoja wa Mataifa iliyopelekwa Lebanon kuchunguza ukweli wa mambo,imesema uchunguzi uliofanywa na Lebanon kuhusu kifo cha Hariri una dosari kubwa.Ripoti hiyo vile vile imeyalaumu majeshi ya Syria kwa ukosefu wa usalama,ulinzi na sheria nchini Lebanon.Rais Emile Lahoud wa Lebanon anaeungwa mkono na Syria ametoa idhini ya kufanywa uchunguzi huru.Walebanon wengi wanailaumu Syria kwa mauaji ya Hariri,lakini balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa,Faisal Mekdad amekataa kuwa nchi yake ilihusika na mauaji hayo.Hariri aliuawa katika mripuko wa bomu uliotokea Beirut,mji mkuu wa Lebanon Februari 14.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW