1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Kikosi cha Umoja wa Mataifa kuongezewa muda Ivory Coast

2 Aprili 2005

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Jumaatatu linatarajiwa kuongeza muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast kwa mwezi mmoja zaidi kutokana na wasi wasi kwamba jitihada za usuluhishi za Umoja wa Afrika yumkini zikakwama.

Mwanadiplomasia mmoja akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema baraza hilo linatarajiwa kuongeza muda wa kikosi hicho kwa mwezi mmoja badala ya kawaida ya miezi sita au mwaka mmoja kuangalia iwapo usuluhishi unaoongozwa na Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini unaweza kuonyesha matunda.

Rais Mbeki anakutana na wawakilishi wa serikali ya Ivory Coast na waasi mjini Pretoria kuzishinikiza pande hizo mbili kutekeleza makubaliano ya amani ya mwaka 2003.

Dai kuu la waasi ni mabadiliko ya katiba yatakayomruhusu kiongozi mkuu wa upinzani Alassane Ouattara kushiriki katika uchaguzi wa Rais unaotazamiwa kufanyika mwezi wa Oktoba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW