1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa maeneo ya ...

12 Novemba 2003
Mmalaka ya Wapalastina yanakaribia kutumbukia kwenye msiba mkubwa wa kibinaadam kufuatia miaka mitatu kukaliwa na Israel. Ripoti hiyo inasema ni nusu ya wakaazi wa Ukingo wa Magharibi na Mwambao wa Gaza wanaoweza kupata chakula mara moja kwa siku. Na sababu kuu ni hatua za Israel kujibu mashambulio ya uripuaji mabomu kwa njia ya kujitolea mhanga na uwekaji vipingamizi dhidi ya Wapalastina. Kiasi wapalastina laki moja wamepoteza kazi zao Israel tangu Septemba mwaka 2000, kwa kuwa wamenyanganywa vibali vya kazi. Na katika maeneo yanayokaliwa na Israel, kazi za kilimo na usafirishaji wa vyakula zinasumbuliwa kwa ukaguzi kwenye vipingamizi majiani na pia sheria ya kukataza watu kutoka nje. Isitoshe kilimo kinaharibiwa kwa njia ya kunyanganya ardhi zenye rotuba.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW