1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Livni asema maadui wa Israel hawatachangia kikosi cha amani Lebanon

17 Agosti 2006

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni, akiwa mjini New York, Marekani, amesema Israel itawakubali wanajeshi wa mataifa ya kiarabu katika kikosi cha kimatafia kitachopelekwa kusini mwa Lebanon, ikiwa mataifa hayo sio adui wa Israel.

Livni ametaka azimio la Umoja wa Mataifa litekelezwe kikamilifu akisisitiza kwamba eneo hilo limelipa gharama kubwa kwa kushindwa kutimizia maazimio yaliyopitishwa awali.

Akizungumza kuhusu juhudi za jami ya kimataifa kuumaliza kabisa mgogoro kati ya Israel na Lebanon, waziri Livni amesema, ´Swala tete sasa ni ikiwa jamii ya kimataifa ina uwezo kuyatekeleza malengo yake. Na sasa huo ndio mtihani na kwa wakati huu jeshi la Israel liko Lebanon.´

Tzipi Livni amesema kutekelezwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa kutasaidia kuleta utulivu katika Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, waziri Tzipi Livni amelaani uamuzi wa Hezbollah kukataa kuwaachilia huru wanajeshi wawili wa Israel akisema ni ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW