1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Marekani kusaidiwa na Umoja wa Mataifa

5 Septemba 2005

Marekani imekubali kupokea msaada wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yalioathirika kwa kimbunga

Katrina.Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa,hivi sasa tume ya kuratibu inakutana mjini Washington kuchunguza vipi juhudi za Marekani zinaweza kusaidiwa.Umoja wa Mataifa upo tayari kupeleka wasaidizi na vitu mbali mbali vya misaada.Mwishoni mwa wiki Ujerumani pia ilipeleka msaada wa dharura kwa mikoa iliyoteketezwa na kimbunga.Siku ya jumamaosi na jumapili ndege za kijeshi za Ujerumani zimepeleka msaada wa chakula katika maeneo ya maafa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW