1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mashtaka ya ulaji rushwa kwenye Umoja wa Mataifa

9 Agosti 2005

Jopo huru linalochunguza mradi wa Umoja wa Mataifa ulioiruhusu Iraq kuuza mafuta ili iweze kununua chakula,limemtuhumu mkuu wa zamani wa mpango huo,Benon Sevan kuhusika na ulaji rushwa.Inasemekana kwamba kutokana na mapato ya mafuta yaliouzwa chini ya mradi huo,Sevan alipokea rushwa.Yeye alijiuzulu kabla ya kutangazwa kwa mashtaka ambayo ameyakana.Kwa wakati huo huo,Alexander Yakovlev,aliekuwa afisa wa kuwadi wa Umoja wa Mataifa amekiri makosa ya uhamishaji wa pesa zisizo halali na kuhusika na njama ya kufanya udanganyifu.Yakovlev alikubali mashtaka hayo baada ya Umoja wa Mataifa,kuondoa kinga yake ya kidiplomasia.Hivi karibuni alijiuzulu kutoka cheo chake cha Umoja wa Mataifa,baada ya kutuhumiwa kuwa alitoa kandarasi ya Umoja huo kwa kampuni iliyomuajiri mwanae wa kiume.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW