1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Mataifa manne kudai viti vya kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

17 Mei 2005

Mataifa manne yameanza hatua zinazolenga katika kujipatia viti vya kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Ujerumani, India, Japan na Brazil zimetoa muswada katika umoja wa mataifa unaotaka kupanuliwa kwa chombo hicho cha umoja wa mataifa kutoka wanachama 15 hadi 25.

Pendekezo lao linataka wanachama wengine sita wapya wawe na uwezo wa kura ya veto kama walivyo wanachama wa sasa wa kudumu, pamoja na wanachama wanne wanaobadilika.

Muswada huo unasema kuwa baraza hilo linapaswa kupanuliwa ili kuweza kuakisi hali halisi ya dunia kwa sasa. Hali hiyo imekuja siku moja baada ya gazeti moja la kila siku nchini Marekani , The New York Times , kuripoti kuwa serikali ya Marekani inatoa ishara kuwa haitaunga mkono suala la kuwa na viti vipya vya kudumu hadi pale mataifa yatakapoacha madai yao ya kutaka kupata uwezo wa kura ya veto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW