1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Mpango wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa kupunguziwa makali

13 Septemba 2005

Ikiwa imebakia siku moja tu kabla ya Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York juu ya kukifanyia mageuzi chombo hicho cha dunia inaonekana kuwa hakuna maendeleo makubwa yaliofikiwa kukidhi dhamira hiyo.

Wanadiplomasia wanajaribu kufikia muafaka juu ya masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na maendeleo,ugaidi na kuzuwiya kuenea kwa silaha za nuklea.Mazungumzo ya dakika za mwisho yaliendelea hadi jana usiku katika juhudi za kukamilisha rasimu ya azimio la Mkutano huo wa Kilele ifikapo leo hii wakati wakuu wa nchi na serikali wakianza kuwasili kwa ajili ya mkutano huo wa siku tatu.

Mataifa yanayoendelea yanataka mikataba mizuri ya biashara na msaada zaidi wakati Marekani na Ulaya zinapambana na kupunguzwa makali kwa masuala ya haki za binaadamu na mapendekezo ya mageuzi ya usimamizi wa shughuli za Umoja wa Mataifa.

Wachunguzi wa mambo wanasema rasimu ya mwisho ya azimio hilo yumkini ikapunguzwa makali mno ya ile tafsiri ya kile alichokuwa nacho mawazoni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Zaidi ya viongozi 170 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Mataifa unaoanza kesho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW