1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Mswaada wa nchi za Kiafrika wa kulipanua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

19 Julai 2005

Nchi za Kiafrika zimewasilisha mswaada mbele ya Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa unaotaka lipanuliwe baraza la usalama la umoja huo. Kama vile lile kundi la nchi nne, Ujerumani, Brazil, India na Japan, nchi hizo za Kiafrika zinataka baraza hilo liwe na wajumbe sita zaidi walio wa kudumu. Kinyume na pendekezo la kundi la nchi nne, mpango wa nchi za Kiafrika unataka nchi hizo sita tangu mwanzo ziwe na kura za turufu. Mazungumzo baina ya pande hizo mbili ili kufikia suluhu hayajafanikwa hadi sasa, lakini yataendelezwa. Ili marekebisho yafanyike katika muundo wa Baraza la Usalama, inahitajiwa kwamba thuluthi mbili ya wajumbe wa Hadhara Kuu wakubali, jambo ambalo sio moja kati ya makundi hayo mawili linaweza kupata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW