NEW YORK : Mzozo wa Palestina haupaswi kusahauliwa
10 Agosti 2006Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameonya kwamba vita nchini Lebanon na kaskazini mwa Israel havipaswi kuondowa nadhari kutoka matukio huko Gaza.
Msemaji wake amesema kwamba mauaji ya raia wakiwemo watoto huko Gaza ni mambo ambayo hayawezi kabisa kuhalalishwa. Watu watatu wameuwawa katika shambulio la Israel hapo jana akiwemo mtoto mmoja.
Israel ilianza operesheni ya kushambulia Gaza mwishoni mwa mwezi wa Juni baada ya kutekwa nyara kwa mwanajeshi wake mmoja.
Wapalestina wanasema zaidi ya watu 170 wameuwawa katika mashambulizi hayo.