1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-york: Nchi 18 za Afrika,Asia na Latin Amerika ...

16 Januari 2004
zinalaumiwa na mashirika yanayopigania haki za binadaam kuendelea kuwatumia watoto vitani.Idadi ya watoto waliotumiwa vitani mwaka jana imeongezeka nchini Ivory Coast,Liberia na katika jamahuri ya kidemokrasi ya Kongo.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya "ushirika dhidi ya kutumiwa watoto vitani" iliyochapishwa na shirika la Amnesty International kwa ushirikiano na Human Rights Watch.Kabla ya hapo mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan,bwana Olara Otunnu alilitaka baraza la usalama liüitishe hatua kali dhidi ya kutumiwa watoto vitani.Taasisi hiyo muhimu ya umoja wa mataifa itakutana jumatatu ijayo kuzungumzia suala hilo.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW