1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Rwanda yataka vitendo sio maneno kuzuwiya mauaji ya halaiki

19 Septemba 2005

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda hapo jana amehoji iwapo viongozi wa dunia wanaweza au la kutimiza ahadi mpya ya kuchukuwa hatua wakati wa mauaji ya halaiki kama yale yalioteketeza nchi yake miaka 11 iliopita.

Mojawapo ya vipengele vilivyopongezwa vya waraka uliotolewa katika mkutano wa viongozi wa siku tatu uliomalizika Ijumaa ni utambuzi wa viongozi wa dunia wa kuwajibika kwa pamoja kulinda watu dhidi ya mauaji ya halaiki,uhalifu wa vita na utokomezaji wa kizazi.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Charles Murigande ameuambia mjadala wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kila mwaka kwamba nchi yake itasubiri kutamka kuwajibika huko ni kwa mafanikio pale mataifa kwa mara nyengine tena yatakapokabiliana na mgogoro wa aina hiyo.

Amesema vitendo na sio maneno kitakuwa kipimo cha mafanikio yao au kushindwa kwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW