1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Sudan yashinikizwa katika Umoja wa Mataifa

21 Septemba 2007

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,Luis Moreno-Ocampo ametoa mwito kwa serikali ya Sudan,kumkamata Ahmed Haroun anaeshukiwa kuhusika na uhalifu katika vita.Haroun ni katibu wa nchi anaehusika na masuala ya kiutu.Afisa huyo wa Sudan anakabiliwa na mashtaka 42 ya uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur.

Ocampo alikuwa akizungumza katika Umoja wa Mataifa mjini New York,kabla ya mkutano wa kimataifa kuhusu Darfur utakaofunguliwa leo Ijumaa.Vile vile,ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuzidi kuishinikiza serikali ya Sudan, kusaidia kuwafikisha mahakamani wale wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu katika vita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW