1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ufaransa imewasilisha azimio katika Baraza la usalama ...

17 Januari 2004
la Umoja wa Mataifa likitaka kupelekwa majeshi ya kutunza amani nchini Ivory Coast. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anafikiria kikosi cha wanajeshi 6 240, lakini Marekani ina mashaka. Hapo awali ilitajwa idadi ni ndogo, - alisema balozi wa kimarekani kwenye Umoja wa Mataifa, John Negroponte. Kama juma moja lililopita, Annan aliliomba Baraza la usalama kuidhinisha ujumbe huo, hata ikiwa pande hasimu zimepiga hatua ya maendeleo kuelekea Amani. Licha ya muwafaka uliokubaliwa mwaka mmoja uliopita, bado kuna hali ya wasiwasi Ivory Coast.