1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Umoja wa mataifa kuunda mahakama ya kimataifa kuwahukumu wanachama wa kikundi cha Khmer Rouge nchini Cambodia.

29 Machi 2005

Karibu miongo mitatu baada ya mauaji ya halaiki yaliyofanyika nchini Cambodia, umoja wa mataifa umepokea kiasi cha Euro milioni tatu ili kuunda mahakama ya uhalifu wa kivita itakayowahukumu wanachama waliohai wa chama cha Khmer Rouge. Katika kikao cha kimataifa cha wafadhili , Japan ilitoa mchango mkubwa zaidi, kiasi cha Euro milioni 16. Kiasi kilichobaki kitatolewa na serikali ya Cambodia. Kiasi cha watu milioni mbili wameuwawa kwa kukosa chakula, kulazimishwa kufanyakazi, magonjwa na kupigwa risasi wakati wa mauaji yaliyofanywa na Khmer Rouge katika mwaka 1975 hadi 1979.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW