NEW YORK : Umoja wa Mataifa kuyakinisha tena kuondoka kwa Syria nchini Lebanon
11 Juni 2005Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameamua kutuma tena nchini Lebanon timu ya Umoja wa Mataifa kuyakinisha iwapo wapelelezi wa Syria bado wangalipo nchini humo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Ikulu ya Marekani kusema kwamba ina habari kwamba serikali ya Syria imeandaa orodha ya viongozi wa kisiasa wa Lebanon inayotaka wauwawe.
Timu hiyo ya Umoja wa Mataifa iliripoti mwishoni mwa mwezi wa Mei kwamba serikali ya Damascus ilikuwa imewaondowa wanajeshi wake wote baada ya kuwepo nchini Lebanon kwa miaka 29.
Lebanon hivi sasa inafanya uchaguzi wa jimbo hadi jimbo ambao unamalizika hapo tarehe 19 mwezi wa Juni huo ukiwa ni uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo katika kipindi cha miongo mitatu bila ya kuwepo kwa wanajeshi wa Syria.