1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa umechangia dollar Billioni 2 na millioni ...

2 Januari 2004
sita kwenye fuko la ujenzi wa Irak. Hii ni kauli ya msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini New York. Fuko hilo linasimamiwa na Marekani ikiwa ni dola inayoikalia nchi hiyo. Fedha hizo zinatoka kwenye mpango wa Mafuta kwa ajili ya Chakula, ambao ulimalizika Novemba. Chini ya mpango huo, kuanzia mwaka 1996 palitarajiwa kupunguza madhila ya wananchi kutokana na vikwazo iliovyoekewa Irak. Pato la mafuta lilitakiwa kununulia bidhaa zinazohitajiwa na wananchi, kama chakula na madawa.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW