1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Umoja wa Mataifa waionya Ivory Coast

12 Machi 2005

Umoja wa Mataifa umeionya Ivory Coast kwamba imekuwa haipigi hatua za maendeleo katika mchakato wake wa amani.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya kulinda amani Jean-Marie Guehenno ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kukwama kwa mchakato huo hivi sasa na hofu ya mashambulizi mapya kunaathiri vibaya sana uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi wa Oktoba.

Tokea mwaka 2002 nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya waasi walioko kaskazini mwa nchi hiyo na vikosi vya serikali vilioko kusini.

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amekuwa akiongoza juhudi za kusitisha mapigano lakini mazungumzo yao yamekwama juu ya namna ya kusalimisha silaha za makundi yanayohasimiana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW