1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Umoja wa Mataifa wamteuwa kamishna mpya wa tume ya wakimbizi.

25 Mei 2005

Umoja wa mataifa umemteua waziri mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres, kuwa kamishna mkuu mpya wa tume ya wakimbizi ya umoja huo.

Anaichukua nafasi ya waziri mkuu wa zamani wa Uholanzi, Ruud Lubbers, aliyeshinikizwa ajiuzulu mwezi Februari kufuatia kashfa ya kuwahujumu wanawake kijinsia, madai ambayo aliyapinga vikali.

Guterres amewashinda watu wengine saba waliokuwa wakikipigania cheo hicho, akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Australia, Gareth Evans.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW