1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Umoja wa Mataifa watafuta suluhu Mashariki ya Kati

11 Agosti 2006

Nchi kuu wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana zimeshindwa kufikia makubaliano yenye lengo la kukomesha mapigano kati ya Israel na Hizbollah na kuifanya Russia kupendekeza usitishaji wa mapigano wa masaa 72.

Balozi wa Marekani John Bolton wakati akikiri kwamba hakuna makubaliano yaliofikiwa amesema bado ana matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano hayo leo hii.Hata hivyo hakuna maudhui yaliowasilishwa rasmi kwenye baraza hilo la usalama la nchi wanachama 15 ambalo linaweza kuchelewesha kupigiwa kura rasimu ya azimio hilo kwa hadi siku moja wakati serikali zikipitia rasimu hiyo.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin amesema kupingwa kwa rasimu hiyo na Lebanon kumezuwiya kufikiwa kwa makubaliano na kwamba atashinikiza kufikiwa kwa suluhu ya haraka ya kibinaadamu katika mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hezbollah.

Zaidi ya Walebanon 1,000 na Waisrael 121 wameuwawa katika mzozo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW