1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Umoja wa Ulaya bado yatumai kutatuwa mzozo wa nuklea wa Iran

16 Septemba 2005

Umoja wa Ulaya bado una matumani kuepuka kufikishwa kwa Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na suala la mpango wake wa nuklea.

Lakini mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Uingereza na Ufaransa pamoja na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York umeshindwa kutatuwa mzozo huo.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer amesema mpira sasa uko mikononi mwa Iran yenyewe.Rais wa Iran anatazamiwa kulizungumzia suala hilo wakati atakapolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo Jumamosi.

Serikali ya Marekani inaishutumu Iran kwa kutaka kutengeneza silaha za nuklea wakati serikali ya Tehran inasema mpango wake wa nuklea ni kwa ajili ya dhamira za amani tu.

Iran imeanza upya shuguli zake za nuklea mwezi uliopita baada ya kuukata mpango wenye vipengele vya vifuta jasho vya kiuchumi uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW