1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: UN kujadili hali ya baadae ya Iraq

13 Januari 2004
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana baadae hii leo kwa majadiliano ya dharura kuhusu Iraq, ikiwa ni pamoja na kuamua iwapo utajuzu kuupokea ujumbe wa serikali ya mpito ya nchi hiyo wiki ijayo. Duru za kibalozi mjini New York zimetaja kuwa kikao hicho kinafanyika kwa ombi la Katibu Mkuu Kofi ANNAN, ambae ameomba majadiliano na wajumbe hao wa serikali hiyo ya mpito mjini Baghdad ili kuafikiana nao jinsi ya kuushirikisha zaidi Umoja wa Mataifa katika harakati za ujenzi mpya wa Iraq. Bwana ANNAN anataka ufafanuzi wa jambo hilo kabla ya Marekani na washirika wake kukabidhi mamlaka kwa serikali hiyo ifikapo Julai mosi mwaka huu. Mwaliko huo umezusha wasiwasi kwa Marekani inayokusudia kuendelea kusimamia harakati hizo licha ya kuongezeka upinzani dhidi ya uvamizi wake nchini Iraq. Ujumbe huo wa Iraq unatarajiwa kuongozwa na Rais wa sasa katika mtindo wa kupasiana madaraka kwa mwezi ambaye ni Adnan PACHACHI.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW