1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Wateja wakosa umeme.

22 Julai 2006

Mjini New York , kukatika kwa umeme ambapo maelfu ya watu wameathirika kumeingia katika siku yake ya tano.

Shirika la umeme Con Edison hapo mapema lilionyesha kuwa hali hiyo haijaathiri eneo kubwa na kudai kuwa wateja wake 2500 ndio wameathirika, lakini jana Ijumaa limeongeza idadi mara kumi zaidi na kufikia wateja 25,000.

Ukosefu huo wa umeme, ambao ulianza siku ya Jumatatu, unakuja wakati New York inakabiliana na joto kali ambalo halijawahi kuonekana kwa muda mrefu wakati wa majira ya joto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW