NEW YORK: Watu milioni 2.5 wakabiliwa na njaa nchini Niger
20 Julai 2005Matangazo
Umoja wa mataifa umesema kwamba Niger inakabiliwa na tatizo kubwa la kibinadamu. Maofisa wa umoja huo na madaktari walio katika taifa hilo la Afrika magharibi wanasema watoto wanafariki dunia kwa sababu ya njaa kwa kuwa ulimwengu umepuuza miito ya kupeleka misaada ya chakula nchini humo.
Mazao ya chakula yalikuwa mabaya mno kufuatia ukame na mimea kuharibiwa na wadudu. Watu milioni 2.5 wanahitaji kwa dharura chakula wakiwemo watoto elfu 800.