1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York:

21 Februari 2005

Kamishina wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Bw. Ruud Lubbers amejiuzulu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amekubali kujiuzulu kwake na amemshukuru kwa majukumu yake. Waziri Mkuu wa zamani wa Uholanzi, aliyeshika wadhifa huo kwa muda wa miaka minne mfululizo amejiuzulu kwa tuhuma kuwa amewalazimisha Wanawake kufanya ngono. Lakini amesisitiza kuwa hana hatia na amechukua hatua hiyo kutokana na shinikizo la vyombo vya habari. Bw. Lubbers ataendelea na wadhifa wake hadi hapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atakapoteua mtu mwingine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW