1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Bush aomba fedha zaidi kusaidia walioathirika na kimbunga Katrina

8 Septemba 2005

Rais George Bush wa Marekani ameliomba bunge kuidhinisha kiasi cha dola milioni 52 za ziada ikiwa ni sehemu ya mpango wa dharura kuendelea kusaidia jimbo lililoharibiwa na kimbunga Katrina.

Fedha hizo ni nyongeza ya dola bilioni 10 kutoka mfuko wa dharura,ambazo zimekwishaidhinishwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wakati huo huo huko New Orleans,watu walionusurika na kimbunga hicho ambao bado wanag’ang’ania katika mji huo, wameamriwa kuondoka mara moja.Maofisa wa afya wamesema maji yaliyochafuka yanaweza kuwasababishia madhara makubwa ya afya.

Kiasi cha watu watano wameshakufa kutokana na maambukizi yaliyotokana na kuchafuka kwa maji.

Pia maofisa wa mji wa New Orleans wameeleza kuwa itawachukuwa muda wa miezi mitatu kuyaondoa maji yote yaliyofurika katika mji wa New Orleans.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW