NEW YORK.Katibu mkuu wa umoja wa mataifa apongeza mapatano ya Hamas na Fatah
9 Februari 2007Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amekaribisha mapatano yaliyofikiwa baina ya Hamas na Fatah juu ya kuunda serikali ya umoja katika eneo la Palestina.
Mapatano hayo yametiwa saini na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal na waziri mkuu Ismail Haniya.
Viongozi kutoka sehemu mbali mbali duniani wamepongeza mapatano ya pande hizo mbili.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier amesema.
O ton…….Napongeza mapatano ya kuundwa serikali ya umoja wa eneo la Palestina. Natumai kwa maafikiano hayo mapigano ndani ya Palestina yatamalizika.
Pia naishukuru serikali ya saudi Arabia na hasa mfalme Abudullah kwa mchango wake muhimu.
Makubaliano hayo yamefuatia mazungumzo yaliyoitishwa mjini Mecca na mfalme Abdullah wa Saudi Arabia.