1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Kigogo wa Iran azishutumu nchi za magharibi kwa kuutumia vibaya umoja wa mataifa

20 Septemba 2006

Mkutano wa 61 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa ulianza vikao vyake hapo jana jioni ambapo viongozi kadhaa walitoa hotuba zao.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan akihutubia baraza hilo kwa mara yake ya mwisho kama katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,

ameonya juu ya hatari iliyopo katika kuenea kwa matumizi ya Nuklia.

Suala la Iran liligubika mkutano huo ,rais Gorge W. Bush wa Marekani amelitaka baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuichukulia hatua Iran baada ya kushindwa kuzingatia mwito wa kuitaka ikomeshe shughuli zake za kinuklia.

Aliwashutumu watu wenye misimamo mikali katika eneo la mashariki ya kati ambao wanachochea ghasia miongini mwa vijana wa eneo hilo.Rais Bush pia amesema nchi za Magharibi hazifanyi kampeini dhidi ya Uislamu lakini inaheshimu dini hiyo.

Lakini akitoa hotuba yake rais wa Iran Ahmed Nejad amesema mradi wa Nuklia wa nchi yake uko wazi, chini ya uangalizi mkubwa wa shirika la Umoja wa mataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA na ni kwa ajili ya matumizi ya amani.

Rais ahmed Nejad amezishutumu nchi za magharibi kwa kuutumia vibaya Umoja wa Mataifa kujaribu kuinyima Iran haki yake ya kuwa na technologia ya Kinuklia huku nchi hizo zikifaidi technologia hiyo.Rais huyo wa taifa la Iran pia ameishutumu Marekani kwa kueneza vita nchini Iraq na kuitetea Israel kuyakalia maeneo ya wapalestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW