New York:Kilimo cha madawa ya kulevya cha pamba moto huko Afghanistan.
3 Septemba 2006Matangazo
Umoja wa Mataifa umeonya kwamba kilimo cha bangi katika Afghanistan kimefikia hali ya juu kabisa. Madawa ya kulevya yaliotolewa na nchi hiyo mwaka huu yanafikiriwa yatazidi kwa karibu asilimia 60, na kufikia tani 6,000. Hiyo ni asilimia 92 ya kima kinachotolewa duniani. Ulimaji wa madawa ya kulevya, hasa yale yanayotokana na Poppy, umetapakaa katika mikoa ya kusini ya Afghanistan. Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema hali ilivyo ni ya hatari, jambo linalozidisha rushwa miongoni mwa polisi na wanasiasa. Umoja wa Mataifa umemtaka Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, aidhibiti hali hiyo ya mambo. Marekani inasema fedha zinazotokana na mauzo ya madawa hayo ya kulevya zinatumiwa kwa ajili ya uasi wa kijeshi.