1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.Lebanon yakataa mswaada wa azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa

7 Agosti 2006

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kuanza tena kujadili mswaada wa azimio kuhusu kusimamisha mapigano baina ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah.

Kupigwa kura juu ya mswaada huo uliopendekezwa na Marekani na Ufaransa kumesimashwa baada ya Urusi na China kupendekeza kuwa mswaada huo unafaa kuongeza vipengele vinavyoivutia Lebanon.

Lebanon imeukataa mswaada huo ambao haui lazimishi Israel kuyaondoa majeshi yake mara moja kutoka ardhi ya Lebanon.

Ujerumani imeuunga mkono huo ambao inasema ni hatua ya kwanza katika kumaliza mzozo wa Israel na Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW