1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Ripoti ya kitabibu juu ya sababu za kifo cha Bwana Arafat.

8 Septemba 2005

Taarifa iliyotolewa na gazeti moja la Marekani la New York Times,imeeleza ripoti ya kitabibu kuhusiana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili aliyekuwa kiongozi wa Wapalestina,Yasser Arafat,haitoi mwanga juu ya kiini cha maradhi yaliyomsababishia kifo.

Katika makala iliyochapishwa leo na gazeti hilo,imeelezwa kuwa dalili za maradhi yake zilikuwa zinaeleka kuwa kiongozi huyo huenda alikufa kwa ugonjwa wa UKIMWI ama alitiliwa sumu.

Ripoti hiyo ni ya kwanza kuzama katika rekodi halisi za kitabibu,tangu Bwana Arafat alipofariki dunia katika hospitali moja mjini Paris,mwezi wa Novemba mwaka jana akiwa na umri mwa miaka 75.

Mjane wa marehamu Arafat,Suha Arafat,ameweka siri juu ya ripoti hiyo ya kitabibu inayoelezea maradhi yaliyokuwa yanamkabili mumewe.

Hata hivyo madaktari wa Kipalestina wanaendelea kusisitiza Bwana Arafat alipewa sumu,tuhuma ambazo maofisa wa Israel wamekuwa wanazikanusha kwa kueleza hazina msingi wowote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW