1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.Sheikha kuongoza hadhara kuu ya UN.

12 Septemba 2006

Kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka 40, hadhara kuu ya umoja wa Mataifa safari hii itaongozwa na mwanamke.

Sheikha Rashid al Khalifa, mwanadiplomasia wa Bahrein anakabidhiwa uongozi wa hadhara kuu ya umoja wa mataifa hii leo.

Wiki moja baada ya kukabidhiwa wadhifa huo, bibi Sheikha Haya Rashid al Khalifa ataongoza mijadala ya hadhara kuu ya umoja wa mataifa itakayohudhuriwa na viongozi wa taifa na serikali kutoka nchi 192 wanachama.

Ujerumani itawakilishwa na waziri wa masuala ya kigeni Frank-Walter Steinmeier.

Hii itakuwa ni mara ya mwisho kwa katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kuhutubia hadhara kuu ya umoja wa mataifa, maana muhula wake wa pili wa miaka mitano madarakani, unamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Mbali na suala nani atachaguliwa kushika wadhifa huo wa ukatibu mkuu, mada kuhusu kufanyiwa marekebisho baraza la usalama na ofisi za katibu mkuu ni mada zitakazojadiliwa na wanasiasa kutoka kila pembe ya dunia hadi September 29 ijayo katika hadhara kuu ya umoja wa mataifa na mikutano mingine ya kimikoa na ya pande mbili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW