1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York:UN yabeza dai la Sudan.

18 Agosti 2006

Umoja wa Mataifa umezibeza lawama nzito juu ya Sudan; Marekani na Uingereza wamesha andaa azimio la kupelekwa wanajeshi wa kulinda amani huko Darfur ambako kumeshashuhudiwa vifo, njaa na maradhi kwa wananchi wa huko.

Umoja huo umependekeza kupelekwa wanajeshi 17,300 kuchukua nafasi za wanajeshi 600 wa umoja wa nchi za ki-Afrika ambao wameshindwa kufanya lolote hadi hivi sasa.

Wanadiplomasia hawana uhakika ikiwa Urusi na China zenye kura ya veto zitakubali azimio hilo na hata hivyo litachukua muda mkubwa kukubalika, maana licha ya Umoja huo kubeza malalamiko ya Sudan, lakini azimio hilo halitakuwa na maana ikiwa Khartoum haitaridhia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW