1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Waandishi wa Marekani waachiwa huru Ethiopea

23 Mei 2007

Waandishi wa habari watatu wa gazeti la New York Times waliyokuwa wakishikiliwa na majeshi ya Ethiopea kwa muda wa siku tano wameachiwa.

Gazeti hilo limesema kuwa waandishi hao akiwemo mkuu wa kituo cha Nairobi, walikamatwa tarehe 16 mwezi huu katika jimbo la Ogaden nchini Ethiopea karibu na mpaka na Somalia.

Limesema kuwa waandishi hao ambao walikuwa kikazi katika eneo hilo walinyanyaswa ikiwa ni pamoja na kupigwa wakati walipokamatwa, ambapo hawakuelezwa sababu ya kukamatwa kwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW