1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Wito watolewa kwa Umoja wa mataifa juu ya suala la Darfur

20 Septemba 2006

Rais Bush wa Marekani ameutolea mwito Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka mzozo wa Darfur ili kukomesha maafa ya kiutu katika jimbo hilo la mgogoro nchini Sudan.

Hata hivyo rais wa Sudan Omar al- Bashir akiwa mjini New-York ameshikilia kupinga kupelekwa wanajeshi wa Umoja wa mataifa huko Darfur,na badala yake amekubali kuongezwa kwa kikosi cha Umoja wa Afrika katika jimbo hilo.

Mwezi uliopita baraza la usalama la Umoja wa mataifa lilipitisha azimio linalotaka kupelekwa wanajeshi hadi 20 elfu wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa katika jimbo hilo kuchukua nafasi ya kikosi cha Umoja wa Afrika ambacho kimeshindwa kuzuia maafa kwenye eneo hilo.

Lakini rais Bashir anawashutumu wale waliolifadhili azimio hilo kuwa watu wenye nia ya siri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW