1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Zealand yafunga shughuli kufuatia visa vya COVID-19

15 Februari 2021

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ametangaza vizuizi vya kufunga shughuli kwa siku tatu katika mji mkubwa wa Auckland baada ya kugundulika visa vitatu vya virusi vya corona.

Neuseeland Neues Kabinett Politik Regierung
Picha: Hagen Hopkins/Getty Images

Hata hivyo visa hivyo visa hivyo bado havijatambuliwa huku baadhi ya mataifa ya Ulaya yakifunga mipaka ili kuzuia kusambaa kwa virusi vinavyobadilika vya coronaWanafunzi wawili Hong Kong waambukizwa kirusi kipya. Hali bado ni tete kufuatia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo vipya. 

Baada ya kikao cha dharura na baraza la mawaziri waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern alisema wameamua kuchukua mwelekeo wa tahadhari hadi pale watakapokuwa na taarifa zaidi kuhusu mlipuko huo. Visa hivyo vitatu vinahusisha mtu na mke wake pamoja na binti yao na ni vya kwanza kugundulika ndani ya taifa hilo tangu Januari 24.

Vizuizi vya kufunga shughuli vinarejeshwa tena kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita nchini New Zealand na kuonekana pigo dhidi ya mafanikio makubwa ya kulidhibiti janga hilo nchini humo.

Alisema, "Kitu kikubwa ninachowaomba watu wa Auckland ni kubaki nyumbani ili kuzuia hatari ya kusambaa. Watu wanatakiwa kufanya kazi kutokea nyumbani, labda tu kama haiwezekani. Kama utatoka nje, tafadhali kaa mbali kwa umbali wa mita mbili ama uko kwenye maeneo yenye usimamizi ambayo unajua kuna  watu wengine, basi ni mita moja."

Kuna wasiwasi kuhusu kufanyika michezo hiyo kutokana na maambukizi ya COVID-19Picha: Jiji Press Photo/dpa/picture alliance

Tukiondoka New Zealand, huko Tokyo Japan, ikiwa imesalia miezi michache ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki, taifa hilo hapo jana limeidhinisha chanjo za BioNTech-Pfizer, ikiwa ni mara ya kwanza kuidhinishwa nchini humo.

Chanjo dhidi ya COVID-19, ilikuwa inaangaliwa kama ufunguo pekee uliosalia wa kufungua kitanzi cha kufanyika kwa michezo hiyo Olimpiki ya majira ya joto, iliyosogezwa mbele.

Ulaya sasa yaanza kufunga mipaka kuzuia kusambaa kwa virusi vipya.

Barani Ulaya, nchini Ujerumani hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vipya vya corona zimeendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufunga mipaka yake na Jamhuri ya Czech na Austria hapo jana, hatua ambayo hata hivyo ilikosolewa na Brussels.

Italia nayo imesema itaimarisha sheria za watu kuingia Austria kuanzia jana Jumapili, na kufanya vipimo pamoja na watu kukaa karantini kwa wiki mbili.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson asifu juhudu za utoaji wa chanjo nchini UingerezaPicha: Jeff J Mitchell/Reuters

Nchini Uingereza, waziri mkuu Boris Johnson amesifu hatua kubwa iliyofikiwa nchini humo ya kutoa chanjo kwa watu milioni 15 kwa miezi miwili tu, baada ya kuanzisha mpango mkubwa wa chanjo. Amesema, Uingereza imefikia lengo lake la kumchanja kila mtu aliyekuwa kwenye makundi manne yaliyopewa kipaumbele.

Bado kuna wasiwasi kuhusu virusi vinavyojibadilisha.

Hata hivyo, washauri wa serikali yake kuhusu masuala ya sayansi wanasema virusi vinavyobadilika vilivyoongezeka nchini humo huenda vikawa vibaya kwa asilimia 70 zaidi ya vilivyopita, na kuelezea wasiwasi zaidi kuhusu virusi hivyo na namna vinavyoweza kubadilisha tabia ya ugonjwa huo.

Ripoti hii mpya inafuatia utafiti uliofanywa na wataalamu wa kundi la maradhi ya kupumua la New Emerging Resipratory Virus Threats Advisory, iliyojikita kwenye tafiti kadhaa zilizogundua virusi vinavyoitwa Kent vilivyoonyesha kuwa ni kitisho zaidi kwa asilimia 30 hadi 70. 

Mjini Geneva, wataalamu wa afya wa shirika la afya ulimwenguni, WHO wanatarajiwa kukutana hii leo kutathmini kuhusu kuthibitisha chanjo ya Oxford-Astra Zeneca, ili iweze kupelekwa kwenye mataifa masikini zaidi.

Soma Zaidi: Tanzania haina mpango wa kuikubali chanjo ya corona

Wataalamu hao walikutana wiki iliyopita kutathmini chanjo hiyo inayotengenezwa Korea Kusini na hii leo wataitathmini inayotenegenezwa na Taasisi ya Serum ya nchini india na majibu yakitarajiwa kutolewa siku zijazo.

DW/AFPE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW