1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Zealand yaonesha wasiwasi misaada ya China kwa Urusi

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa New Zelandand, Nanaia Mahuta ameelezea wasiwasi wake kuhusu China kuipa msaada wa silaha Urusi iliyo katika vita na Ukraine

Neuseeland Wellington | APEC Meeting
Picha: APEC NEW ZEALAND/REUTERS

Ofisi ya waziri huyo wa mambo ya kigeni wa New Zealand imetoa taarifa juu ya mkutano wa Mahuta alioufanya Beijing siku kadhaa baada ya Rais wa China Xi Jinping kukamilisha ziara yake mjini Moscow.

Soma zaidi:China yakosoa ripoti kuhusu ukiukaji, Xinjiang

Akizungumzia vita inayoendelea Ukraine, Mahuta amelaani uvamizi wa Urusi wakati alipozungumza na waziri mwenzake wa wa mambo ya kigeni wa China, Qin Gang. Katika mazungumzo hayo, Mahuta alionesha pia wasiwasi wake kuhusu hali ya haki za binadamu katika eneo la Xinjiang, kuzorota kwa uhuru Hong Kong na mizozo katika bahari kusini mwa China.

Chanzo: AFPE