NEWYORK: Korea yashinikizwa zaidi kurejea kikaoni juu ya silaha za kinuklea
24 Machi 2005Matangazo
Rais Gorge Bush ameitolea wito Korea kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo juu ya mpango wake wa kinuklea. Hata hivyo rais Bush amekanusha kuweka siku ya mwisho ya kurejea mazungumzo hayo kuwa mwezi Juni.
Bush aliyasema hayo baada ya kuarifiwa zaidi na waziri wake wa mambo ya nje Condolezza rais aliyekuwa ziarani barani Asia.
Korea kaskazini imesema itarejea katika mazungumzo hayo iwapo tu masharti kadha yatatimizwa.
China iliyokuwa mwenyeji wa mazungumzo yaliyosambaratika pia imezidisha shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini wakati wa ziara ya waziri mkuu wake Pak Pong Ju huko Beijing.