1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK: Vikwazo dhidi ya Khartoum

3 Machi 2005
Wakimbizi wa Sudan nchini Chad.
Wakimbizi wa Sudan nchini Chad.Picha: dpa

Maseneta wawili wa bunge la Marekani wameutaka Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo vikubwa serikali ya Sudan ili kumaliza mauaji yanayofanyika katika eneo la Darfur.

Katika mswada uliowasilishwa kwenye bunge la Marekani,senata Sam Brownback wa chama cha Republican na Jon Corzine wa chama cha Demokrat wameitaka serikali ya Marekani kulishawishi baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya kimataifa dhidi ya serikali ya Khartoum.

Wamemtaka pia rais Gorge Bush kuwataja wajumbe maalum watakaoshughulikia mzozo wa Darfur.

Watu elfu 70 wameuwa na mamilioni ya wengine kulazimika kuhama maskani yao miaka miwili iliyopita kufuatia mashambulio yaliyokuwa yakitekelezwa na wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya Khartoum.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW