Neymar atakiwa kufika mahakamani
3 Aprili 2015Kituo kimoja cha redio kimesema kuwa “kulingana na duru za kisheria, waendesha mashtaka watamtaka afike kama shahidi katika kesi ya kukwepa kulipa kodi dhidi ya rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, klabu hiyo na rais wa zamani Sandro Rosell.
Waendesha mashtaka wa Uhispania wanaomba vifungo vya miaka miwili na miezi mitatu jela dhidi ya rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na miaka saba dhidi ya Sandro Rosell, kuhusiana na sakata la Neymar
Mahakama ya Madrid pia inata klabu hiyo itozwe faini ya euro milioni 22.2. kuhusiana na uhamisho wa Neymar ambayo umekuwa ukifanyiwa uchunguzi wa ufisadi.
Barcelona ilisema ililipa jumla ya euro milioni 57 ili kuipata sahihi ya Neymar kutoka klabu ya Santos nchini Brazil, lakini jaji anashuku kuwa kiasi kamili cha fedha kilikuwa zaidi ya euro milioni 83.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu