Ngao ya Jamii: Yanga ama Simba?
15 Septemba 2025
Historia haitoshi kuamua nani atashinda Pambano hilo la Ngao ya Jamii kwani kila mechi ya Ngao ya Jamii huleta ushindani wa hali ya juu, na mara nyingi mafanikio hutoka kwa maandalizi, morali ya timu, na mikakati ya kocha.
Kocha wa Simba Fadlu Davis ametoa kauli hii kuelekea mchezo huo.
"Tumekuwa na maandalizi mazuri kabla ya msimu na tuko tayari Bila shaka, kuna wachezaji wengi wapya, pamoja na wachezaji wa msingi ambao wamebaki Kwa hivyo tuko na hamu kubwa kuona msimu unapoanza na nani anaweza kucheza Derby Tuna hamu kubwa kwa mchezo huu na ni mtihani mkubwa kwetu Sio kwetu tu bali pia kwa wachezaji wadogo Mabingwa wawili wakubwa wakikabiliana uso kwa uso tunaweza hkutegemea mchezo wa kusisimua"Amesema Kocha wa Simba Kocha wa Simba Fadlu Davis
Beki wa Simba Shomari kapombe amesema wachezaji wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo.
"Tmefanya maandalizi Vizuri na tumepokea mafunzo mengi kutoka katika benchi letu la ufundi utakuwa ni wakati mzuri kuelekea katika mchezo huu na sisi kama wachezaji tupo Tayari "Amesema Beki wa Simba Shomari kapombe.
Ushindani utakuaje?
Kwa upande wa Yanga kocha Romain Folz anabainisha kuwa mechi hiyo itakuwa ya ushindani.
"Tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza katika nafasi hiyo Naweza kukuhakikishia kwamba yeyote nitakayemchagua kuanza au kuingia kwenye mchezo kesho atafanya vizuri Atatoa kiwango kizuri Iwe ni Balla cont'e , iwe ni Aziz, hata Duke anaweza kucheza katika nafasi hiyo Tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza pale Wote wana uwezo wa kutoa kiwango kizuri Kwa hivyo kwangu mimi"Amesema Kocha mkuu wa yanaga Romain Folz
Beki wa Yanga SC, Dickson Job amesema ni wajibu wa wachezaji kupambana ili kupata matokeo.
"kwa niaba ya wachezaji sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo kwani tunaamini utakuwa mchezo mgumu lakini sisi kama wachezaji ni wajibu wetu kwenda kupambana kupata matokeo"Amesema Beki wa Yanga SC, Dickson Job
Mashabiki wa Simba na Yanga wamezungumzia kuelekea mchezo huo.
"Mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii inaenda kwa upande wetu simba sports klabu tunaenda kulipa kisasi hatuwezi kukaa kinyonge kwa muda mrefu ''Amesema shabiki wa Simba Augstino Madehe
"Kwa upande wangu mimi kama shabiki wa Yanga naiona ni mechi ambayo itakuwa ni tafu kwa sababu Timu zote zimejipanga ni mechi itakuwa ngumu kwa uwanjani"Amesema shabiki wa Yanga Mussa Nangale
Pambano hilo muhimu litachezwa saa 11 jioni kwa saa za Tanznaia katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuashiria ufunguzi wa msimu wa ligi kuu soka Tanzania Bara katika msimu wa 2025/26.